HIZI NDIZO SIFA ZA MWANAUME ANAYEMTAKA SHILOLE | BONGOJAMII

HIZI NDIZO SIFA ZA MWANAUME ANAYEMTAKA SHILOLE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Zuwena Mohamed ' Shilole' anayetamba na hit ya 'hatutoi kiki' amefunguka na kudai kwamba haitaji kuolewa na mwanaume mwenye pesa kwani wengi wao hutumia mali zao kama fimbo ya kuwachapa na kunyanyasia wanawake zao.


Akiwa Kikaangoni kwenye ukurasa wa Facebook wa EATV, Shilole amefunguka kuwa yupo tayari kuolewa lakini mpaka atakapo pata mwanaume atakayekidhi vigezo vyake huku akitaja pesa siyo kitu anachokitanguliza bali heshima, upole na ukarimu.


"Natamani sana kuolewa lakini mpaka nimpate mtu mwenye vigezo ninavyohitaji mimi, napenda mwanaume anayejali, atakayeniheshimu lakini awe pia anafanya kazi kama hafanyi kazi simtaki. Lakini pia wanaume wenye pesa siwataki maana tunawaona huko majumbani wanavyotumia kama fimbo kuwanyanyasa wake zao" Shilole alifunguka.


"Mimi siangalii sana muonekano kwani unaweza kutengenezwa lakini ukiwa mfupi mimi sitakukubali nahitaji mwanaume mrefu na mwenye heshima na anayejituma kwenye utafutaji" aliongeza Shilole.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts