MAAMUZI YA KAMATI YA MAADILI KUHUSU PAUL MAKONDA | BONGOJAMII

MAAMUZI YA KAMATI YA MAADILI KUHUSU PAUL MAKONDA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge hilo.


Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.


Aidha, Kamati ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka ya bunge.


Pia Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kudharau mamlaka ya bunge.


Hata hivyo, Bunge limeazimia kumsamehe mbunge huyo baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha .


Katika hatua nyingine,Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa karipio kali na Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts