Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MSHAMBULIAJI Antoine Griezmann ameamua kubaki Atletico Madrid msimu ujao na kumaliza tetesi za kuhamia Manchester United kwa dau la Pauni Milioni 86.
Mpachika mabao huyo wa Kifaransa, kwa kiasi kikubwa amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford, lakini baada ya Atletico kufungiwa kusajili wachezaji wapya inaonekana amemaliza tetesi hizo.
Jana jioni kwenye ukurasa wake wa Twitter, Griezmann aliweka picha yake akiwa amevaa jezi ya Atletico ikiwa imeambatana na maelezo yasemayo: "Sasa zaidi kuliko daima#Atleti #WotePamoja'
Tayari Man United imekwishasitisha mpango wa kumchukua mchezaji huyo na kuanza kuangalia namba 9 mwingine, huku wachezaji kama Romelu Lukaku wa Everton na Alvaro Morata wa Real Madrid wakipewa nafasi ya kuziba pengo la mkongwe Zlatan Ibrahimovic.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka