IGP SIRRO KUKUTANA USO KWA USO NA WAZEE WA RUFIJI, KIBITI | BONGOJAMII

IGP SIRRO KUKUTANA USO KWA USO NA WAZEE WA RUFIJI, KIBITI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dar es Salaam. Siku moja baada ya wakazi wa wilaya za Kibiti na Rufiji kumtaka azungumze na wazee, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amekubali wito huo na kwamba wiki ijayo atakwenda huko na kuzungumza nao.

Katika ziara hiyo mkoani Pwani, Sirro amesema baada ya kupokea taarifa kutoka kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, ataonana na kufanya mazungumzo na kamati hiyo, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza na Mwananchi jana, Sirro alisema amepanga kutembelea maeneo hayo ili kuzungumza na wananchi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ili kutafuta suluhisho la mauaji yanayofanyika katika wilaya hizo.

“Nimepokea wito wao, nitakwenda huko wiki ijayo baada ya kupokea taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama. Lazima nizungumze na wananchi kwa sababu ni wadau muhimu wanaotusaidia polisi,” alisema Sirro.

Alisema ni jambo zuri kwa wananchi kuona umuhimu wa kushirikiana na jeshi la polisi katika kutafuta suluhisho kwa matatizo yanayowakabili na kwamba amekubali wito huo kwa sababu ilikuwa ni dhamira yake tangu alipoapishwa.

Wakazi wa maeneo ya Kibiti na Rufiji walisema Sirro akikaa na kuzungumza na wazee atapata sababu za mauaji ya viongozi wa vijiji.

Takribani watu 31 wameuawa tangu Mei 31, 2016 wengi wao wakiwa ni viongozi wa vijiji na vitongoji. Mfululizo wa mauaji hayo pia uliwahusisha askari polisi ambao waliuawa na watu wasiojulikana.

Tukio la kuuawa kwa polisi wanane waliokuwa doria lilizua taharuki zaidi katika ukanda wa Mkoa wa Pwani.

Mei 29, Rais John Magufuli alimwapisha Kamishna Sirro kuwa IGP mpya akichukua nafasi iliyoachwa na Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kazi kubwa iliyo mbele ya Sirro ni kukomesha mauaji ya wananchi katika mkoa huo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts