KIMENUKA, MBUNGE JOHN HECHE KUHAMASISHA WANANCHI KUZIPIGA MAWE NDEGE ZA ACACIA | BONGOJAMII

KIMENUKA, MBUNGE JOHN HECHE KUHAMASISHA WANANCHI KUZIPIGA MAWE NDEGE ZA ACACIA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefunguka na kusema kwa kuwa Rais Magufuli kupitia ripoti ya pili ya mchanga amesema kampuni ya ACACIA ni feki na haipo basi yeye anawaambia wananchi wa jimbo lake wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu.


Heche amesema hayo bungeni jana na kudai kuwa atasimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa ndege za kampuni hiyo zikitua mgodini kwa ajili ya kubeba madini basi zinapigwa mawe kwa kuwa wananchi wa jimbo lake la Tarime ambapo hiyo migodi ipo wameumizwa sana kusikia hiyo kampuni inayochukua mali zao ni feki na hewa.


"Kampuni ile ya ACACIA Rais amesema feki na hakuna 'formula' ya kukamata mwizi mlisema wenyewe, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye sisi hatutaruhusu madini yatoke pale ndege ikitua itapigwa mawe, magari yao tutayakamata kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. 


"Mhe. Spika sisi tulitegemea Mhe. Rais aseme madini yasiondoke nchini mpaka mambo hayo yote yapitiwe, tutazuia mchanga madini yanaondoka. 


"Rais amesema ACACIA ni mwizi wewe unataka utaratibu wa kukamata mwizi Tarime, sisi watu wetu wameumia sana na maji ya sumu, ng'ombe wamekufa, watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa pale mgodini"alisema Heche


Mbali na hilo John Heche alisema kuwa kama serikali itamkamata kwa maamuzi ambayo atafanya basi Watanzania watajua kuwa serikali haipo tayari kupigana vita hii ya kupigania rasilimali za nchi hii, hivyo amewataka watu wa jimbo la Tarime wajiandae na kuanza maandalizi ya kupigania rasiliamali zao ili waone kama serikali itapeleka jeshi la polisi kulinda mali za wezi hao. 

==>Msikilize Hapo chini akiongea

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts