MBOWE AKANUSHA SAUTI INAYOSAMBAA MTANDAONI KUWA WEMA SEPETU NI MPENZI WAKE | BONGOJAMII

MBOWE AKANUSHA SAUTI INAYOSAMBAA MTANDAONI KUWA WEMA SEPETU NI MPENZI WAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Habari inayotikisa mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile Audio (voice note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.


Leo kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM Mbowe ameielezea sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka: 


“Mimi nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema kwa sababu siyo za kweli.


“Timu yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu. 


"Sauti siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za upotoshaji tu."

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts