Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mteule Anna Elisha Mghwira leo Juni 6, 2017 saa 3:30 asubuhi hii Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Anna Mghwira anaapishwa leo baada ya kuteuliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Said Meck Sadick aliyeomba kujiuzulu.
Hadi wakati huu hakuna taarifa rasmi iliyokuwa imetolewa na Chama cha ACT Wazalendo kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wao, na wala mteule huyo hajazungumza jambo lolote.
Rais @MagufuliJP atamuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mteule Anna Mghwira leo June 6, 2017 saa 3:30 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.— Msemaji wa Serikali (@TZ_MsemajiMkuu) June 6, 2017
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka