Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Meneja uendeshaji wa mradi Mhandisi Lydia Ndibaleme akimuonesha Mkuu wa Mkoa Paul Makonda mchoro wa ramani wa mradi huo utakao jengwa katika eneo la Jangwani Jijini Dar es salaam
SERIKALI mkoani Dar es Salaam, imetangaza kujenga miradi mitatu mikubwa ya maji itayo maliza tatizo la uhaba wa maji jijini humo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Maonda, ametembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na Mamlaka la Maji safi na Majitaka mkoani Dar es Salaam (DAWASA).
Miradi hiyo ni pamoja na ile ya uondoaji na usafishaji wa majitaka, miradi wa uboreshaji huduma za usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Pia miradi ya uchimbaji wa visima katika wilaya ya Ubungo.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa kukagua maendeleo ya shuughuli mbalimbali za ujenzi wa miradi mipya iliyo na lengo la kumaliza tatizo la majisafi na maji taka katika jiiji la Dar es Slaam.
Huu ni muendelezo wa ziara zake alizo anza hivi karibuni ambapo tayari ametembelea chanzo kipya cha maji Kimbiji wilayani Kigamboni ambako kuna miradi ya uchimbaji wa visima virefu vyenye urefu wa kina cha mita 600 na miradi iliyokamilika ya upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu na Chini mkoani Pwani.
Mradi wa ujenzi wa mitambo mitatu mikubwa na ya kisasa ya kusafisha majitaka itakayo kwenda sabamba na ulazaji maboomba ya ukusanyji maji taka itajengwa katika eneo la Jangwani, Mbezi beach na Kurasini ili kuongeza kiwango cha` kusafisha majitaa cha asilimia 10 cha sasa kufikiaa asilimia 30 ifikapo mwaa 2020.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mradi tenki la maji eneo la Mabwepande Dsm
Gharma za jumlaza miradi hii ni dola milioni 600.
Miradi hii inatekelezwa kwa awamu tatu, na awamu ya kwanza inaanza ndani ya mwaka huu wa fedha 2017/18.
Mradi wa mfumo wa majitaka jangwani unahusu ujenzi wa mtambo wa kusafishia majitaka ambapo ukapokamilika utakuwa n uwezo wa kusfisha mta za ujazo 200,000 kwa siku.
Mfumo wa mabomba yenye urefu wa kilomita 376 yatakay9lazwa kuanzia Ubungo hadi Jangwani, Kinondoni, Mwananyamala mdsasani na katikati ya jiji utajengwa.
Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco Cyprian Luhemeja (Kulia) akimuelezea Mkuu wa mkoa Paul Makonda namna mradi huo utakavyomaliza tattizo la maji Jijini Dar es salaam endapo utakamilika
Awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha sehemu itakayoweza kusafisha mita 2500 kwa siku na mabomba ya kilomit 17.43 yataakayojengwa katikaa eneo la magomeni.
Pia katika awamu ya kwanza bomba linalomwaga majitakaa baharini litaacha kutumika na badala yake majitaka hayo yatasafishwa kwa kutumia mtambo huo.
Mtambo huo unajengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na korea kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya exim ya korea.
Unatarajiwa kugharimu dola za marekani milioni 90. Taratibu za ununuzi zinaeendelea ili kumpata mshauri na hatimye mkandarasi lengo likiwa ni kuanza ujenzi mapema mwaka 2018.
Mfumo wa majitaka mbezi utjengwa kilongwima na utakuwa na uwezo wa wa ,kusafisha mita za ujazo 16000 kwas iku . utajengwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na benki ya dunia kupitia mkopo wa masharti nafuu na unatarajiwa kugharimu dola milioni 65.
Ujenzi wa mtambo wa kusafisha maajitaka kurasinini utakuwa na mfumo wenye urefu wa kilomita 90 utakaolazwa katia maeneo ya changombe , kurasini, temeke na uwanja wa taifa.
Mradi huo utajengwa kwa kushirkiana na shirika la maendeleo la ufaransa afd na utakuwa na uwezo wa kusafisha mita za ujazo 11,0000 kwa siku.
Mitambo hiyo itawezesha kuzaisha gesi asilia na umeme kwaajili ya kuendeshea mkitambo hiyo hivyo kupunguza matumizi ya gharama za umeme na vilevile maji yatakayokuwa yametbiwa yatauzwa na kutumika katika shughuli mbalimbali kama ile kupoozea mitambo na umwagiliaji.
Tope litakaobakibaada ya mchkato huo wa usafishaji majitaka litaweza utmika kama mbolea kwaajili ya kilimo panja na bustani za majani na miti ya kivuli na hivyo kupendezesha jiji.
Pamoja na miradi hiyo mradi mwingine ni wa uboreshaji mfumo wa usambazaji maji ambao unahusisha ujenzi wa matenki tisa ya kuhifadhia maji na kusambaza maji yenhye ukubwa wa kuhifadhi lita za ujazo milioni tatu hadi milioni aita.
Meneja uendeshaji wa mradi Injinia Lydia Ndibaleme akizungumza na Waandishi wa habari katika ziara hiyo jinsi ambavyo wata utekeleza mradi huo namna ambavyo wananchi watanufaika kwa kiasi kubwa Pwani na Jijini Dar es salaam.
Pia ujenzi wa vituo vine vya kusukum maji, ununuzi wa transifoma, na ufungaji njia za umeme wa msongo wa mkubwa na ulazaji mabomba makubwa ya ugawaji maji na mabomba ya usambazaji maji yataayokuwa na urefu wa kilomomita 477.
Maeneo yanayotarajiwa kunufaika na mradi huo ni changanyikeni, bagamoyo,mpiji, zinga , kiromo , kitopeni ukumi kerege buma mataya na ukanda maalumu ya eoz
Lengo la mradi huu ni kuhakikisha wananchi wote wa kawaida wenye viwanda na bashara katika eneo lote la mradi wanapat huduma bora za maji hasa baada ya maji kuongezeka kufuatia kukamilika kwa kazi zaupanuzi wa mitamb ya maji ya ruvu juu na ruvu chini.
Mradi huo utgharimu dola za marekani milioni32 kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya inda.
Pia mradi wa uchimbaji wa visima katika manispaa ya ubungo ili kuwapunguza changamoto wakati miradi mikubwa ya usambazaji maji ikisubiriwa kutekelezwa.
Mkataba ulisainiwa aprili 11,2017 na unatarajiwa kuisha agosti 31, 2017 mbapo visima 10 viatarajiwa kkuchimbwa ambapo utagharimu shilingi milioni109.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka