KITIMTIM, MIFUKO 400 YA MAGENDO YA SUKARI YAKAMATWA | BONGOJAMII

KITIMTIM, MIFUKO 400 YA MAGENDO YA SUKARI YAKAMATWA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekamata mifuko 400 ya sukari iliyokuwa ikisafirishwa kwa magendo.


Taarifa ya mamlaka hiyo imesema mifuko hiyo ya sukari ya kilo 50 kila mmoja imekamatwa usiku wa kuamkia jana, Agosti 26 ikiwa imepakiwa kwenye magari mawili aina ya Mitsubishi Fuso.
TRA imesema hatua hiyo ni mwendelezo wa kampeni yake ya kukamata magendo, kazi inayofanywa na kikosi chake maalumu cha Fast kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama.


Mamlaka hiyo imesema mzigo huo na watuhumiwa wa magendo wanaodaiwa kuwa ni sugu wamekamatwa eneo la Bagamoyo mkoani Pwani.


Taarifa imesema magari hayo ya mizigo yanashikiliwa katika ghala maalumu la TRA kwa hatua za kisheria, ikiwemo kuyataifisha.


Imeelezwa mzigo huo ni wa hatari kwa kuwa hauna vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).


TRA imewaomba wananchi kutoa taarifa za vitendo kama hivyo ili kukomesha dhuluma kwa nchi na uwezekano wa afya zao kudhurika.


MCL

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts