MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFAA DHIDI YA KESI YA UGAIDI YA MBUNGE WILFRED LWAKATARE | BONGOJAMII

MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFAA DHIDI YA KESI YA UGAIDI YA MBUNGE WILFRED LWAKATARE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mahakama ya Rufaa Tanzania imeyafuta maombi ya kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kutaka kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kufuta shtaka la ugaidi lililokuwa linamkabili Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.

Maombi hayo yamefutwa na Jaji Mussa Kipenka baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka kueleza kwamba DPP ameamua kuondoa kibali cha maombi hayo kwa sababu hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kutokana na hatua hiyo Lwakatare ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA anakabiliwa na kosa moja la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky kwa kutumia sumu ambalo kesi hiyo ipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts