Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa Polisi katika mji wa Nairobi, Japheth Koome
Machafuko yaibuka Kenya, watano wapigwa risasi
WATU 5 wamepigwa risasi katika ghasia zilizotokea nchini Kenya baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi nchini Kenya, anaandika Hellen Sisya.
Ghasia hizo zimetokea jana baada ya kinara wa kambi ya upinzani, Raila Odinga kudai kuwa kumefanyika udanganyifu mkubwa.
Mkuu wa Polisi katika mji wa Nairobi, Japheth Koome amesema watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi jana akisisitiza kuwa walitumia machafuko kupora mali za watu.
Mtu mwingine aliuawa mapema jana kwa kupigwa risasi na polisi katika kaunti ya Kisii nje ya Shule ya Sekondari ya Nduru ambayo ilikuwa na kituo cha kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la uchaguzi la Mugirango.
Katika mji wa Kisumu ambao ndiyo ngome kuu ya kinara wa upinzani Raila Odinga, polisi ilitumia gesi ya kutoa machozi na risasi kutawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi wa rais.
Matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) yanaonesha kuwa, mgombea wa chama cha Jubilee, Uhuru Kenyatta anaongoza kwa kura milioni 7.9 sawa na asilimia 53.89 ya kura zilizohesabiwa huku mpinzani wake mkuu, Raila Odinga akiwa na kura 6.5 sawa na asilimia 44.47 ya kura.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha NASA, Raila Odinga amepinga matokeo hayo akisema yamechakachuliwa.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka