VURUGU ZINGINE ZAIBUKA KENYA, WAFUASI WA WAGOMBEA WACHOMA MOTO SOKO | BONGOJAMII

VURUGU ZINGINE ZAIBUKA KENYA, WAFUASI WA WAGOMBEA WACHOMA MOTO SOKO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Sehemu ya soko kuu mjini Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya, imeteketea baada ya mfarakano kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa ugavana katika kaunti hiyo.

Fujo zilizuka baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne kutangazwa.

Ali Bunow Korane wa chama cha Jubilee chake Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.

Taarifa zinasema watu wasioridhishwa na matokeo hayo walichoma moto sehemu za soko hilo.

Hali ya utulivu imerejea lakini wazima moto wameendelea kukabiliana na moto huo.

Korane alipata kura 55 335 (51,48%) naye mpinzani wake wa karibu Nathif Jama Adan wa chama cha Wiper akapata kura 50 471 (46,95%).

Bw Adan ndiye gavana anayeondoka.



Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts