Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Tanga. Wakuu wa mikoa iliyopo Kanda ya Kaskazini wamejiwekea mkakati endelevu wa kukagua mafuta kwenye vituo vilivyopo maeneo yao ikiwa ni kufanyia kazi agizo la Rais John Magufuli aliyetaka mafuta yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Tanga yauzwe kwa bei ya chini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Agosti 11 jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela alisema yeye na wenzake, Joel Bendera wa Manyara, Anna Mghwira wa Kilimanjaro na Mrisho Gambo wa Arusha wameweka mkakati wa pamoja wa kuendesha ukaguzi wa kila kituo chapetroli, dizeli na mafuta ya taa kujua kama yanauzwa kwa bei inayolingana na yalikotolewa.
“Hili la mafuta tayari mimi na mwezangu, Bendera, Mghwira na Gambo tumeshaanza kufanyia kazi tangu jana (Alhamisi) ukaguzi unaendeshwa na tutahakikisha tunapita vituoni kujiridhisha kama wauzaji wa mafuta
wanayauza kwa bei ya Tanga au ya kutoka Dar es Salaam,” alisema Shigela.
Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa maghala ya Kampuni ya GBP Jijini Tanga, Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa
mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kufanya ukaguzi kwenye vituo vya mafuta kuhakikisha yanayotolewa Tanga yanauzwa kwa bei ya chini kuliko ya Dar es salaam.
Alisema ameamua kutoa agizo hilo ili uwekezaji uliofanywa na kampuni
ya GBP jijini Tanga wa maghala ya kupokea mafuta kutoka nchi za Uarabuni yaweze kuuzwa kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini na hivyo kuondoa msongamano katika Bandari ya Dar es salaam.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka