HATIMAYE MTANZANIA KUKIPIGA LA LIGA | BONGOJAMII

HATIMAYE MTANZANIA KUKIPIGA LA LIGA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
KIUNGO wa klabu ya Deportivo Tenerife, Farid Mussa, amesema hivi karibuni Watanzania watamuona akicheza katika Ligi Kuu ya Hispania maarufu ikiitwa La Liga.

KIUNGO WA KLABU YA DEPORTIVO TENERIFE, FARID MUSSA.

Farid yuko hapa nchini akiitumikia timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo leo inatarajia kuikaribisha Botswana katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mussa, alisema kuwa tayari ameshapandishwa kutoka timu ya vijana na sasa wakati wowote anaweza kuanza kucheza Ligi Kuu Hispania endapo kocha atampanga.

“Karibu nitaanza kucheza katika Ligi Kuu ya Hispania, nimechelewa kuanza kwa sababu kwanza nilisajiliwa katika timu ya vijana, ila baada ya kuonyesha uwezo mzuri nimepandishwa na kuwa kwenye timu ya wakubwa, timu yetu inafanya vizuri na tunamshukuru Mungu tumeshinda mechi mbili za kwanza," alisema Mussa.

Kiungo huyo wa zamani wa Azam FC ya jijini Dar es Salaam alisema jana kuwa bado ataendelea kupambana kuhakikisha anapata namba ya kudumu kwenye klabu yake na hatimaye kupandisha thamani yake kwenye ligi hiyo.

Aliongeza kuwa anaamini kufanya kwake vizuri ndiyo kutawavutia mawakala wa timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu Hispania na nchi nyingine za Ulaya kwa ajili ya kumsajili.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts