Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Akizungumza, Msuva alisema kwamba walikuwa wana mechi ngumu jana kwa sababu walikutana na wapinzani wazuri.
“Ilikuwa mechi ngumu sana, jamaa wazuri sana, lakini tutajitahidi tushinde mechi ya marudiano kwao tusonge mbele,”alisema Msuva.
Mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola kati ya Difaa Hassan El – Jadida na FUS Rabat uliokuwa ufanyike leo Uwanja wa FUS, Hay Nahda mjini Rabat umeahirishwa.
Difaa sasa watasafiri kuifuata Ittihad Tanger Septemba 20 kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la FA.
Wakati huo huo: Simon Msuva amekanusha uvumi kwamba yeye ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa klabu yake, Difaa Hassan El- Jadida.
“Kaka hizi habari mimi sijui hata zinatoka wapi, hakuna kitu kama hicho. Ni habari za uongo,”amesema Msuva.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka