ROMA MKATOLIKI AIBUKIA KENYA | BONGOJAMII

ROMA MKATOLIKI AIBUKIA KENYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rapa Roma Mkatoliki

Rapa Roma Mkatoliki ambaye amerudi na ujio wa nguvu na ngoma zake 'Zimbabwe' na 'Hivi ama vile' baada ya kukaa kimya muda mrefu baada ya kupata matatizo ya kutekwa sasa ameibukia nchini Kenya.

Roma Mkatoliki pamoja na Stamina ambao kwa pamoja wanaunda umoja wao unaofahamika kwa jina la 'Rostam' wameanza kupiga hatua mbele zaidi ya kutangaza muziki wao na kuwafikia mashabiki nje ya Tanzania baada ya wakali hao kuonekana nchini Kenya wakifanya 'Media tour' 

Umoja wa Roma Mkatoliki na Stamina unafahamika zaidi pindi wakali hao wanapokutana kwenye jukwaa moja na kutoa burudani kwa mashabiki kwani kwa uwezo wao huwa wanaweza kuamsha mashabiki na kutoa burudani ya nguvu.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts