ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE DAR SIKU TANO KUANZA JUMATANO | BONGOJAMII

ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE DAR SIKU TANO KUANZA JUMATANO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Takriban Madaktari 200 kutoka katika hospitali za serikali, hospitali binafsi pamoja na taasisi za kiafya wataendesha zoezi la Upimaji wa Afya bure kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwa siku tano kuanzia Jumatano Septemba 6 hadi Septemba 10 katika viwanja vya mnazi mmoja .

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaambia waandishi wa habari pamoja na baadhi ya madaktari kutoka hospitali za serikali na za Binafsi kwamba taratibu zote za zoezi hilo zimekamilika hivyo amewahamasisha imiza wananchi kujitokeza katika zoezi hilo ambalo litakuwa na madaktari bingwa.

Baadhi ya Magonjwa yatakayohusika katika upimaji huo ni pamoja na Tezi Dume, kansa ya titi na shingo ya uzazi, shinikizo la damu pamoja na magonjwa yote yasiyopewa kipaumbele ambayo yamekuwa yakisababisha athari kubwa kwa binadamu. Aidha Bwana Makonda ameelekeza kutolewa tiba bure kwa wale watakaobainika kusumbuliwa na magonjwa.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts