ACHANA NA HARMORAPA, HUYU APA WEMARAPA...ADAI WEMA SEPETU ANAJIPENDEKEZA KWAKE | BONGOJAMII

ACHANA NA HARMORAPA, HUYU APA WEMARAPA...ADAI WEMA SEPETU ANAJIPENDEKEZA KWAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Kuna imani kuwa duniani wawiliwawili! Hii inajidhihirisha kwa mwanadada Lisa Deedee `Tuerny’ ambaye amejipatia umaarufu mitandaoni kutokana na kufananishwa na staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu.


Kupitia gazeti hili, mrembo huyo anafunguka mambo mbalimbali usiyoyajua kuhusu yeye; Ijumaa: Hivi Tuerny ulijuaje kuwa unafanana na Wema?


Tuerny: Nakumbuka mwaka 2012 niliweka picha mtandaoni, mama akanitumia sms kwamba ninafanana na Wema, nilishtuka lakini tangu hapo akawa kama amebariki hicho kitu. Nilishangaa kila sehemu niliyokwenda watu wananiambia nafanana na Wema.


Ijumaa: Ulijisikiaje kufananishwa naye na ni changamoto zipi unazokutana nazo?


Tuerny: Sikuona kama ni kero, nilichukulia kawaida tu, haikuwa chanzo cha mimi kufanya vitu vya kufanana naye, mimi siyo mtu wa shobo kama hao wengine na sijawahi kuwa shabiki wake, changamoto ni kwamba wengi wanajua Wema ni ndugu yangu wakati si kweli.


Ijumaa: Je, umeshawahi kuwa na ukaribu na Wema?


Tuerny: Sijawahi na sifikirii, ila kipindi watu wanaanza kunifananisha naye alifurahi akawa ana-comment kwenye picha zangu Instagram, akawa ananisifia na mimi ninamjibu, lakini kutokana na maneno ya watu akachukia na kunipotezea.


Ijumaa: Kwa nini hupendi awe rafiki yako?


Tuerny: Yeye ana marafiki wengi na kwenye maisha yangu sipendi kuwa na mtu mwenye marafiki wengi, kwani majungu yatakuwa mengi.


Ijumaa: Nilisikia kuna kipindi uliwahi kukutana na Wema lakini ukampotezea hata salamu hukumpa, kwa nini?


Tuerny: Ni kweli, mwaka 2015 nikiwa kwenye mishe zangu nilimuona pale Klabu Cafee, akatabasamu na mimi pia, tatizo mimi sijui kujipendekeza ndiyo maana sikumfuata.


Ijumaa: Vigogo wangapi ambao wamewahi kukuomba penzi, kwa kutaka kuonja ladha ya copy ya Wema?


Tuerny: Inawezekana watu wanaumiza kichwa kwa sababu hiyo, lakini wanashindwa kunifuata kutokana muonekano wangu, mimi ni kauzu zaidi ya dagaa.


Ijumaa: Uliwahi kukumbwa na kashfa ya kutoka kimapenzi na Romy Jones, ilikuwaje?


Tuerny: Sijawahi kuwa naye, watu walizusha kwa sababu zao binafsi.


Ijumaa: Mfano Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ sukari ya warembo, akikutokea utakubali?


Tuerny: Hahaa siwezi, kuwa na mwanaume mpaka nimpende siyo tu kwa sababu yeye ni f’lani.


Ijumaa: Ni mwanaume wa aina gani anakidhi vigezo kuingia naye kwenye uhusiano?


Tuerny: (anacheka) awe mrefu, mwenye bodi na anajielewa, yaani asiwe mtu wa kuongea sana, maana sipendi mtu muongo.


Ijumaa: Kuna mastaa ambao wameshawahi kukuomba penzi na ulishawahi kutoka na wangapi?


Tuerny: Wapo wengi wanaoshoboka, huwa nawapotezea na siwezi kuwataja kwa sababu sipendi kujikweza.


Ijumaa: Je, una ndoto ya kuwa msanii wa filamu au muziki au video queen?


Tuerny: Mmh, kuwa video queen hapana labda mtu anilipe si chini ya milioni saba, kuhusu filamu labda niwe dairekta, ila ndoto yangu kubwa ni kuwa mwanamuziki, naamini itatimia ‘soon’.


Ijumaa: Unajishughulisha na nini, kinachoweza kukukwamua kimaisha?


Tuerny: Nina saluni yangu inaitwa T flawless ipo Magomeni-Mikumi ninapoishi, yaani make up studio, napamba maharusi na watu wa kawaida.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts