RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA) | BONGOJAMII

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA)

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 25 Machi, 2017 amemteua Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Kabla ya Uteuzi huo Bw. Charles Edward Kichere alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.


Bw. Charles Edward Kichere anachukua nafasi ya Bw. Alphayo Kidata ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.


Kufuatia uteuzi huo, nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA itajazwa baadaye.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


25 Machi, 2017

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts