HATIMAYE WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI WASSITISHA MGOMO | BONGOJAMII

HATIMAYE WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI WASSITISHA MGOMO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe (Katikati) akizungumza na wanahabari.

UMOJA wa Wamiliki wa Vyombo Vya Usafiri (TABOA) wametangaza kusitisha mgomo wao uliyokuwa ukitarajia kuanza kesho Aprili4,2017.


Akitangaza uamuzi huo mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TABOA, Mustapha Mwalongo amesema uamuzi huo umefikiwa kufuatiwa kuwepo na mazungumzo baina ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbalawa mapema hii leo na kufikiana mwafaka juu ya walichokuwa wakihitaji.

Makamu Mwenyekiti wa TABOA, Abdallah Mohammed naye akifafanua Jambo.

Aidha amesema serikali kupitia kwa Waziri Mbalawa itarekebisha kanuni na taratibu ikiwemo makosa na adhabu stahiki baina ya madereva na wamiliki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe alisema anashukuru kwa uamuzi huo walioufikia wa kusitisha mgomo wao kwani ungeliweza kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi.

GPL

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts