Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Wachezaji wa timu ya Simba na Toto (Picha na Maktaba).
KESHO Jumamosi kikosi cha Simba kitashuka kwa mara nyingine kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kupambana
na Toto Africans baada ya Jumatatu iliyopita kuitembezea kichapo Mbao FC mabao 3-2.Hata hivyo, mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo amezua balaa jijini humo baada ya uongozi wa Toto Africans kudai kuwa hauna imani naye.
Mmoja wa viongozi wa Toto ambaye aliomba kutotajwa jina lake gazetini, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, mwamuzi Jacob Adongo ambaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimpatia onyo kali baada ya kushindwa kutafsiri vizuri sheria katika mechi ya Simba dhidi ya Mbeya City, ndiye amepangwa kuchezesha mechi yao.
Alisema kutokana na hali hiyo hawana imani naye kwani wanahofia kuwa yale aliyoyafanya katika mechi ya Simba na Mbeya Citykwenye Uwanja wa Taifa, Dar anaweza kuyafanya tena dhidi yao.
“Kusema kweli hatuna imani naye na tayari tumeshawaambia TFF kuhusiana na hilo,” alisema
kiongozi huyo.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum
Chama, alisema: “Kila mwamuzi anayechezesha ligi tunamuamini, sioni haja ya wao kulalamika.”
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka