SIKU YA LEO IWE FARAJA KWA ROMA NA WENZAKE | BONGOJAMII

SIKU YA LEO IWE FARAJA KWA ROMA NA WENZAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Saikolojia ya Roma Mkatoliki na wenzake bado ipo kwenye hali ya kuteswa na kutekwa alikotendewa hivi karibuni na watu wenye nia ovu.
Namkumbusha Roma Mkatoliki na wenzake Bin Laden pamoja Monii kuwa hata Yesu Kristo siku kama ya leo alikuwa amepatiwa mateso makali kutoka kwa wayahudi wenye maono ya kiudharimu na wasiopendezwa na haki.

yesu alitendewa hayo yote kutokana ukumbozi kwa watu wengine ili kusimama kwenye kuamini ujumbe wake.
Roma ni Msanii mwenye kupaza sauti za wanyonge na kuzungumzia sana masuala yanayohusu maslahi ya umma hivyo kama ulitekwa kwa sababu hizo upo kwenye njia ya yesu.
Nakumbuka vibao vyako na mashairi yako kadhaa ambayo uliimba kwa uchungu na uzalendo bila kutafuna maneno uliimba kuhusu mustakabari masuala kadhaa.

Hukuacha kupaza suati kukemea ufisadi tangu uliponza kazi hii ya sanaa kupitia muziki wa Hip Hop.
Roma itoshe tu kujikubali kuwa wewe ni Mwanakondoo uliyepitia mtihani huu na kwamba wanaobeza kitendo ulichofanyiwa wewe yatwakuta tumerithi misemo kutoka ka malenga wetu isemayo ukimuona mwenzako ananyolewa nawe tia maji kchwa chako,

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts