Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Thabit Abdul.
WAMILIKI wa Makundi ya Taarab, Thabit Abdul wa Wakali Wao na Said Fella wa Yah TMK nusura wazichape msalani kisa kutaka kuchukuliana wanamuziki. Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika onyesho la pamoja la bendi hizo ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar.
Wawili hao walikutana msalani wakati Fella akitoka na Thabit akiingia ndipo songombingo lilipoanzia huku Thabit akimlalamika Fella kuzungumza na wanamuziki wake akiwalaghai kuwachukua.
Hata hivyo, songombingo hilo liliwahiwa na mashabiki kuingilia kati na kuwaachanisha. Baada ya kutulia kwa tafrani hiyo, Over Ze Weekend lilimsogelea Thabit na kumhoji kulikoni:
“Fella ameniudhi sana, alikuwa akizungumza na baadhi ya wanamuziki wangu kwa lengo la kuwashawishi wajiunge naye,,” alisema Thabit.
Fela.Naye Mkubwa Fella alisema: “Siwezi kumfanyia unyambilisi wa kumwibia wanamuziki, najua alipotokea na namchukulia kama mwanangu tu wala asipaniki.
Source: Global Publisher
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka