SERENGETI BOYS YAKABIDHIWA RASMI BENDERA YA TAIFA KWA AJILI YA MICHUANO HUKO GABON | BONGOJAMII

SERENGETI BOYS YAKABIDHIWA RASMI BENDERA YA TAIFA KWA AJILI YA MICHUANO HUKO GABON

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) leo tarehe 3 Aprili 2017 ameshiriki kwenye zoezi la kuwaaga na kuwapatia bendera ya Taifa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).

Mhe. Mwakyembe amewaasa vijana wa Serengeti kuliwakilisha vyema Taifa kwenye michuano ya AFCON wanayotarajia kwenda kushiriki hivi karibuni.

Mhe. Mwakyembe akiongozana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi aliwahakikishia vijana wa Serengeti utayari wa Serikali katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Vilevile, Mhe. Mwakyembe ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuwachangia Serengeti Boys ili waweze kuwa na ushiriki bora katika michezo ya maandalizi nchini Morroco na Cameroun na baadaye katika michuano ya AFCON, nchini Gabon.

Sambamba na hilo Mhe. Mwakyembe aliwaongoza wananchi waliofika uwanja wa Taifa kuishangilia Serengeti boys iliyokuwa ikicheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya vijana kutoka Ghana, ambapo Serengeti boys wameweza kurudisha magoli mawili na matokeo hadi mwisho yakawa sare ya 2-2.

“Mpira umemalizika tumetoka sare ya 2-2. Mechi ilikuwa ngumu na ni zoezi zuri kwa Serengeti Boys. Tuzidi kuwatia hamasa,” amesema Malinzi mara baada ya mchezo huo leo jioni.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts