HATIMAYE MBWANA SAMATTA APANDA THAMANI | BONGOJAMII

HATIMAYE MBWANA SAMATTA APANDA THAMANI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Thamani ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta imepanda katika soko la wachezaji duniani.

Thamani yake kwa imefikia kiwango cha Euro milioni 3 sawa na shilingi bilioni 7.1 za kitanzania kwa mujibu wa mtandao unaohusika na biashara za wachezaji duniani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Samatta kutimiza idadi ya kiwango cha magoli iliyokuwa ikihitajika ambapo ameweza kufunga mabao saba katika mechi sita za hivi karibuni akiwa katika timu yake ya Genk pamoja na mawili aliyoyapachika Botswana mchezo uliochezwa na Taifa Stars

Mabadiliko hayo yamefanyika mwishoni mwa mwezi Machi ambapo mshambuliaji huyo alionekana kung'ara katika ushindi wa bao 4-1 iliyopata klabu yake dhidi ya Lokeren na yeye akitupia bao mojawapo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts