Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Sanga aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni 68 (7) pamoja na 64 A,B,C, alisema ndani ya Bunge yameongelewa mambo yanayohusu mahakama, usalama, mauaji na kutekwa.
“Nilikuwa nadhani kupitia kanuni hizi naomba mwongozo wako nini kazi ya Bunge mheshimiwa naibu spika?” alihoji.
Mwongozo huo uliibuka baada ya Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Angelina Malembeka kuwataka wabunge waliosema kuna orodha ya wabunge 11 wanaotakiwa kutekwa kuwataja majina yao.
Hoja ya Malembeka ilimlenga Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ambaye siku za karibuni aliliambia Bunge kwamba ameambiwa na mmoja wa mawaziri kuwa kuna wabunge 11 watatekwa na Usalama wa Taifa.
Hata hivyo, mwongozo wa spika ulioombwa na Sanga ulizima kiu ya Malembeka aliyetaka kumbana Bashe ataje majina ya wabunge hao 11, badala ya kutaja idadi pekee. Akijibu mwongozo wa Sanga, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliamua kupiga marufuku masuala ya Usalama wa Taifa kujadiliwa bungeni.