AFA MAJI AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUMUOKOA MWENZAKE ZANZIBAR | BONGOJAMII

AFA MAJI AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUMUOKOA MWENZAKE ZANZIBAR

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Zanzibar. Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya kuzama katika mto wa maji maeneo ya Kibonde Mzungu wakati akiwa katika jithada za kumuokoa mpanda pikipiki aliyezama mtoni hapo baada ya kusombwa na maji ya mvua inayoendele kunyesha visiwani Zanzibar.

Hilo ni tukio la pili kutokea maeneo hayo kutokana na athari ya mvua inayoendelea kunyesha visiwani humu, ambapo hivi karibu Askari Polisi anayefahamika kwa jina la Abbasi Anasi (55) amefariki dunia maeneo hayo hayo kutokana na kusombwa na maji wakati akipita na Vespa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali alimtaja kijana huyo kuwa ni Mohamed Abdalla Ali (32) mkazi Fuoni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Alisema kuwa tukio hilo limetokea saa nne za asubuhi, ambapo marehemu huyo alikuwa katika jithada za kumuokoa mpanda pikipiki anayefahamika kwa jina la Paulo Salum (40) aliyezama mtoni hapo kwa kusombwa na maji ya mvua wakati akipita.

Alisema kuwa mpanda pikipiki huyo pamoja na jitihada za kujiokoa asiingie katika mto huo lakini maji yalikuwa na kasi kubwa na kupelekea kushindwa nguvu hatimaye kuingia yeye pamoja na chombo chake.

Kamanda Nassir alisema kuwa marehemu huyo baada ya kumuona mwenzake huyo kuzama kwenye maji hayo alionyesha uzalendo wa kuingia kwenye mto huo ili kumuokoa lakini naye alishindwa kutoka.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts