Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Lindi. Kiongozi wa mbio za mwenge, Amour Amour ametakaa kukagua mradi wa kikundi cha vijana changamkia fursa cha ufugaji wa nyuki jimbo la Mtama (VICHASCO)baada ya viongozi wa kikundi hicho kutoa taarifa za uongo ikiwemo umri wao.
Mradi huo unaojumuhisha vijana zaidi ya 15 wanaofanya shughuli za kufuga nyuki , utengenezaji wa thamani na ufyatuaji wa tofali umeshindwa kukaguliwa baada ya watendaji kutoa taarifa zisizo sahihi.
Awali kabla ya kukaguliwa mradi huyo wanakikundi wajilitambulisha kwa kiongozi wa mbio za mwenge ndipo alipoanza kubaini kuwa anadanganywa baada ya mwenyekiti wa kikundi hicho Mohamedi Magongo (38) na Mnole Hasani (37) kudanganya umri wao kuwa wao ni vijana wakati umri wao umepita ujana.
Amour amesema utambulisho wa kikundi unaonyesha kuwa ni kikundi cha vijana lakini baadhi ya wanachama na viongozi wa kikundi wana umri mkubwa uliopita wa ujana.
Amesema ameshindwa kukagua mradi huyo kutokana na kutoridhishwa na taarifa za awali zilizotolewa na viongozi wa kikundi ambazo tayari zimempa wasiwasi kuwa hata taarifa zingine zitakuwa za kupikwa.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka