ALIYEFARIKI KWENYE AJALI YA MKUDE ,MWILI WAKE WAREJESHWA NYUMBANI KWAO | BONGOJAMII

ALIYEFARIKI KWENYE AJALI YA MKUDE ,MWILI WAKE WAREJESHWA NYUMBANI KWAO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MWILI wa marehemu Shose Fidelis upo njiani unarejeshwa nyumbani kwao, Dar es Salaam kutoka mkoani Morogoro.
Shose amefariki dunia mchana wa leo muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, kufuatia ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Binti huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 na ushei, alikuwa pamoja na Nahodha wa Simba, Jonas Mkude kwenye gari hilo na watu wengine, wakitokea Dodoma, ambako jana timu yao ilitwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri.
Ndani ya gari hilo walikuwepo pia wapenzi wengine wa Simba, Jasmin na Faudhia ambao wameumia na wamelazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro na hali zao ni mbaya.
Mkude amerejeshwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi, wakati dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba yupo chini ya uangalizi wa Polisi

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts