WARITHI WA MHONGO KUJILIKANA HIVI KARIBUNI | BONGOJAMII

WARITHI WA MHONGO KUJILIKANA HIVI KARIBUNI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Rais John Magufuli, anatarajiwa kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa ili kujaza nafasi ya waziri wa Nishati na Madini.


Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Profesa Sospeter Muhongo kung’olewa katika wadhifa huo Mei 24, kutokana na ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais, kuchunguza mchanga wa dhahabu katika makontena 277.


Kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ilisema kampuni ya Acacia, haikutangaza kiasi cha madini yote yaliyokuwa katika makontena 277 ambayo yalizuiwa kusafirishwa nje kwa amri ya Rais.


Matokeo ya kamati hiyo yanaonyesha kuwa thamani ya madini yote yaliyopo kwenye makontena 277 ni kati ya Sh829.4 bilioni na Sh1.439 trilioni, tofauti na thamani iliyotolewa na Acacia ya Sh97.5 bilioni.


Hii ni mara ya pili kwa Profesa Muhongo kung’olewa katika wizara hiyo. Januari 24, 2015 alijiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ikiwa ni shinikizo la Bunge, baada ya kutolewa kwa maazimio ambayo pamoja na mambo mengine, yalitaka mamlaka ya uteuzi wake imwajibishe.


Vyanzo mbalimbali vimedokeza kuwa Rais Magufuli hana jinsi zaidi ya kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri ili kujaza nafasi hiyo huku wanaofaa kumrithi wakitajwa.
“Unajua bajeti ya wizara hii inakuja Alhamisi na Ijumaa ijayo, kwa hiyo hapa katikati tunatarajia kuwapo na mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri,” kilidokeza chanzo chetu.


Chanzo hicho kilisema Rais anaweza kufanya moja kati ya mambo mawili, ama kuteua waziri wa Nishati na Madini bila kupangua wengine au kufanya pia mabadiliko ya baraza lake.


“Anaweza akateua waziri wa Nishati na Madini akaishia hapo. Lakini anaweza pia kutumia fursa hiyo kuboresha baraza lake la mawaziri kwa kufanya mabadiliko madogo,” alisema.


Majina yanayotajwa kumrithi Profesa Muhongo, ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts