BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AMTEUA SIMON SIRRO KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI | BONGOJAMII

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AMTEUA SIMON SIRRO KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2017 amemteua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Kabla ya Uteuzi huo IGP Simon Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa kesho Jumatatu tarehe 29 Mei, 2017 saa 3:30 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Mei, 2017

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts