BAD NEWS: TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI SITA VIWANGO VYA FIFA | BONGOJAMII

BAD NEWS: TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI SITA VIWANGO VYA FIFA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), jana Alhamisi lilitoa viwango vya soka vya mwezi Julai kwa mataifa mbalimbali ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi sita kutoka 114 ya hadi 120.

Wakati kimataifa Tanzania ikishika nafasi ya 120, kwa upande wa Afrika ipo nafasi ya 35, huku ikiwa ya nne katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda inaongoza ikifuatiwa na Kenya, kisha Rwanda na Burundi inaburuza mkia. Katika nafasi kumi za juu kwenye orodha hiyo, Brazil inaongoza ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Uswizi, Poland, Ureno, Chile, Colombia, Ubelgiji na Ufaransa inahitimisha.


Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts