WIMBO MPYA WA ROMA MKATOLIKI WAZUA MASWALI MENGI KWA MASHABIKI | BONGOJAMII

WIMBO MPYA WA ROMA MKATOLIKI WAZUA MASWALI MENGI KWA MASHABIKI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Katika wimbo huo Roma Mkatoliki amejaribu kuhusisha matukio mbalimbali ya kisiasa pamoja na lile la kwake kubwa la kutekwa ambapo hii ndiyo kazi yake ya kwanza tokea ule mkasa wake wa kutekwa kuisha na kusababisha maumivu mengine makali kutoka kwa mashabiki zake baada ya kuona 'video' yake mpya iliyojaa hisia kali za maumivu.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa 'youtube' alioweka video hiyo mpya watu zaidi ya 668 wametoa maoni yao jinsi walivyoupokea ujio mpya wa Roma na hizi ni baadhi tu ya zile zilizoandikwa na mashabiki wa Roma.

Pharergy Ramson: "Roma ukienda Zimbabwe harakat atazifanya nani 'but' ngoma iko poa hujawahi kuniangusha ila umebadirika kidogo mzee. Nadhan kwenye hii ngoma umejibu maswali ya watu wengi sana kipindi unafanya 'show' pale 'Dar live' nilitamani urudie hii nyimbo 'but' sikuwa na uwezo ila umefanya vizur."

Blandina Bilau: "Simjui sana Roma wala kufuatilia nyimbo zake lakini huu wimbo umeniliza, 'message' imefika jipe moyo. Mtetezi wako Mungu aendelee kukutetea"
Arthur Oyaro: "Duuh 'so sad' na utu uzima huu machozi nimeshindwa kuyazuia,'thank' pia kwa kunifikirisha. Viva Roma viva''

Mdachi Classic: "Nimefatilia 'comment' nyingi sana ila sijaona hato komenti inayozungumzia vibaya hii ngoma zaidi ni za upendo na za kuumizwa tu. 'In short' hii imetugusa sana pole sana kaka yupo mungu hakimu wa yote".

Ibrahim Utenga: ''This song reflects the real prevailing situation, it's very sensitive song, congratulations to you brother, God save you "

Ndongo Nyambalya: "Nina wasiwasi wewe Mkatoliki hicho siyo kichwa ni semi-computer, kwenye Mungu wa John na Daud hapo nimefikiria hadi najikuta nurudiarudia kusikiza, U deserve bro! Gat u! 100".

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki amemwagiwa sifa kedekede na mashabiki zake ambao walikuwa wamemisi kusikia na kuona kazi zake kwa kipindi kirefu tokea alipopatwa na mkasa wa kutekwa miezi michache iliyopita na kuweza kurudi katika uhalisia wake bila ya kuhofia jambo lolote litakaloweza mtokea tena mbele yake kwa ukali wa tungo zilizojaa za kufikirika.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts