WAPIGADEBE KUPANDISHWA KIZIMBANI | BONGOJAMII

WAPIGADEBE KUPANDISHWA KIZIMBANI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
JESHI la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema linaendelea na operesheni ya kuwakamata wapigadebe huku idadi kamili ya waliokamatwa ikitarajiwa kutangazwa Ijumaa.

Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Lucas Mkondya aliliambia Nipashe jana kuwa, moja ya adhabu watakayopewa waliokamatwa ni kufikishwa mahakamani.

Mkondya alisema kwa sasa operesheni inaendelea na ikifika siku ya Ijumaa atatangaza idadi yao.

Alipoulizwa mara baada ya kuwakamata watawafanya nini, Kamanda Mkondya alisema watawafikisha mahakamani na alipoulizwa kwa makosa gani, Mkondya alisema: “Siyo kila kitu kiandikwe gazetini’.”

Operesheni ya kukamatwa watu hao inatokana na kuripotiwa matukio 20 hadi 50 ya wizi kwenye vituo vya daladala jijini huku wapiga debe wakidaiwa kuwa kichaka cha wizi huo.

Awali, Kamanda Mkondya aliliambia gazeti hili kuwa, baada ya kuwaondoa wapiga debe na wizi ukaendelea vituoni, watawaondoa pia watu wote ambao hawana shughuli maalum.

Machi 16 mwaka jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha anawaondoa wapigadebe wote kwenye vituo vya mabasi kwa sababu hizo hizo.

Agizo hilo alilitoa wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa yote nchini ambao walikuwa wameapishwa na Rais John Magufuli, Ikulu siku iliyotangulia.

Katika mafunzo hayo, Waziri Simbachawene alisema kupiga debe sio kazi rasmi na isiyo na kipato kitakachoweza kumkwamua kijana husika kuondokana na umaskini.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts