Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kocha mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina.
KOCHA mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amefunguka kuwa makosa madogomadogo wanayoyafanya safu yake ya ulinzi yanampa presha kuelekea mchezo wao Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, ambayo ina safu iliyoshiba ya ushambuliaji inayoongozwa na Mganda, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda.
Lwandamina na kikosi kizima cha Yanga kwa sasa kipo kisiwani Pemba, kilipoweka kambi yake ya kujiandaa na mchezo huo wa Ngao ya Jamii, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Agosti 23, mwaka huu.
Safu ya ulinzi ya Yanga inaongozwa na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Andrew Vicent ‘Dante’ pamoja na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ imeonekana kutokuwa vizuri kwa siku za hivi karibuni.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mzambia huyo amesema kuwa ameona udhaifu kwa mabeki wake hao wa kati baada ya michezo kadhaa ya kirafiki lakini atapambana nayo kabla ya mechi hiyo dhidi ya Simba. “Kuna makosa baadhi nimeyabaini kwenye kikosi changu hasa kwenye safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikifanya makosa madogomadogo ambayo nahitaji kuyarekebisha kabla ya mechi yetu dhidi ya Simba.
“Naamini hadi tukamilishe kambi yetu ya huku Pemba basi kila kitu kitakuwa sawa kwa kurekebisha dosari hizo na hadi tukirudi Dar, kila kitu kitakuwa kimeshakaa kama vile ninavyotaka kwani nimepanga kuwapa mbinu ambazo zitawafanya wawe bora zaidi, najua Simba ina washambuliaji hatari kama Okwi na wengine hivyo hatutakiwi kufanya makosa mengi,” alisema kocha huyo.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka