HANS POPO APEWA JUKUMU ZITO , KUWATENGENEZEA YANGA SUPU YA MAWE | BONGOJAMII

HANS POPO APEWA JUKUMU ZITO , KUWATENGENEZEA YANGA SUPU YA MAWE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Bosi wa Simba, Zacharia Hans Poppe.
HARAKATI za mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu zinaendelea, bosi wa Simba, Zacharia Hans Poppe amepewa jukumu la kuhakikisha Yanga wanapata kichapo.

Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba amepewa majukumu hayo lakini siyo ambayo yanahusiana na mambo ya ufundi wa ndani ya uwanja yanayofanywa na benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Mcameroon, Joseph Omog.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameliambia Championi Ijumaa kuwa: “Hatutaki mchezo kabisa sa­fari hii, tunachotaka ni ush­indi kwa hiyo tumeamua kumkabidhi komandoo wetu, Zacharia Hans Poppe majukumu maalumu ya ku­fanya ili tuweze kuibuka na ushindi.

“Kila mtu ndani ya Simba anajua kuwa Hans Poppe siyo mtu wa mchezomche­zo kwa hiyo tunaamini kuwa atawaandalia Yanga supu ya mawe siku hiyo,” alisema Manara.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts