MASAU BWIRE AINGILIA KATI MECHI YA SIMBA NA YANGA , ADAI NI MECHI YA KITOTO | BONGOJAMII

MASAU BWIRE AINGILIA KATI MECHI YA SIMBA NA YANGA , ADAI NI MECHI YA KITOTO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema watu hawana raha mitaani kwa kuwa gumzo pekee ni Yanga na Simba kwa kuwa zinakutana kesho.

Lakini akasisitiza, timu hizo hazina lolote kwa kuwa zina mambo ya kitoto kwa kuwa huwa hazionyeshi soka lolote zaidi gumzo la mazoea.

Yanga na Simba zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya Ngao ya Jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Masau ambaye ni mwalimu kitaaluma, amesema hakuna kipya ambacho timu hizo huwa zinaonyesha.

“Nikuambie hawa jamaa hawana lolote hasa kama unazungumzia uwanjani. Mimi naona ni mambo ya kitoto tu, gumzo kubwa kila sehemu mtaani hadi hatuna raha.


“Lakini ukienda uwanjani pale, hakuna kiwango chochote kinachoonyeshwa,” alisema.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts