AMBER LULU AWEKA HADHARANI MAHUSIANO YAKE NA BABA YAKE | BONGOJAMII

AMBER LULU AWEKA HADHARANI MAHUSIANO YAKE NA BABA YAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii wa bongo fleva Amber Lulu amefunguka na kudai hayamsumbui maneno anayotupiwa na watu mitandaoni kwa yeye kupiga picha za nusu uchi kwa kuwa mtu pekee anayemuhofia hayupo katika mitandao hiyo.

Amber Lulu ameeleza hayo kupitia eNewz ya EATV baada ya kuandamwa kwa kipindi kirefu akiwa na watu kuhusu kupiga picha akiwa mtupu na kuweka katika mitandao ya kijamii jambo ambalo lilisababisha baadhi ya watu kudhani mrembo huyo pengine hana wazazi ndiyo maana anajitoa akili kwa kupiga picha za aina hizo.

"Dingi nashukuru Mungu siyo mtu wa kufuatilia sana mitandao ya kijamii hasa Instagram 'maybe' aone gazeti na kwenye we abahatishe sana, siyo mtu mfuatiliaji. Kwa hiyo vitu vingi vinakuwa vinapita havijui", alisema Amber Lulu.

Pamoja na hayo Amber Lulu aliendelea kwa kusema "Baba yangu anafahamu ninapokaa, siyo kwamba nimetoka huko sijaaga. Niko vizuri yaani nimetoka huko nilipokuwa na baraka zote ndiyo maana naweza kufanya kitu na Mungu naye akaweka baraka zake na nikaweza kum-move on hizo zote ni baraka zake"

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts