Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
BODI ya Ukurugenzi ya Azam FC imemteua Mwanasheria na msomi, Shani Christoms kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu, nafasi iliyooachwa wazi na Nassor Idrissa Mohammed 'Father'.
Awali, Shani alikuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu na katika mabadiliko haya, nafasi yake inachukuliwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
Akitangaza mabadiliko hayo mbele ya vyombo vya habari leo, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti, Nassor Idrissa Mohamed ‘Father’ sasa anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa bodi.
Alisema kuwa bodi hiyo pia imemteua Shani Christoms kuwa Mwenyekiti mpya wa Azam FC, ambaye awali alikuwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo.
Aidha kwa mujibu wa mabadiliko hayo, nafasi ya Christoms imezibwa na bodi hiyo kwa uteuzi wa Abdulkarim Mohamed Nurdin ‘Popat’, ambaye amewahi kuwa mchezaji wa timu hiyo wakati Azam FC ikiitwa Mzizima.
Mbali na kuichezea timu hiyo, pia amesomea mafunzo ya ukocha na mwanzoni mwa mwaka huu alisomea mafunzo ya uongozi wa soka.
Idd alimalizia kwa kusema katika kuboresha safu ya uongozi wa timu hiyo, bodi hiyo imemteua Abdul Mohamed, kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC na kukifuta cheo chake cha awali cha Meneja Mkuu.
Wengine wanaounda sekretarieti hiyo ya Azam FC, ni Meneja wa timu, Phillip Alando na Ofisa Habari, Jaffar Idd.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka