Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo tarehe 22 Agosti 2017 amekabidhi jumla ya milioni 23 kwa familia za watoto Doreen, Wilson na Sadia ambao walikuwepo nchini Marekani kwa matibabu kufuatia ajali mbaya ya gari waliyopata mwezi wa tano mwaka huu.
Mrisho Gambo amepata nafasi ya kukutana na familia za watoto hao pamoja na watoto wenyewe na kudai kuwa kupitia watoto hao na uponywaji wao ameona utukufu wa Mungu
"Leo nimekutana na familia za wazazi wa watoto Sadia, Doreen na Wilson ambao watoto wao walinusurika na ajali ya basi ya Lucky Vicent Mkoani Arusha. Aidha, tumewakabidhi 7,750,000 kila familia ili ziwasaidie kwenye masuala yao mbalimbali pamoja na Elimu. Nimeona utukufu wa Mungu kupitia watoto hawa" alisema Mrisho Gambo
Watoto Doreen, Wilson na Sadia wamerejea nchini Tanzania kutokea nchini Marekani siku ya Ijumaa ya tarehe 18 Agosti 2017 na kupokelewa na wananchi mbalimbali katika uwanja wa KIA akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine mbalimbali pamoja na baadhi ya wasanii wa injili akiwepo Mercy Masika kutoka Nairobi pamoja na Angel Bernard
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka