Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii wa mwenye 'hit song' ya 'anameremeta', Nuh Mziwanda ameanza kupoteza muelekeo wa maisha yake kiujumla kutoka na kutendwa kipenzi mpaka kufikia hatua ya kuomba msaada katika mitandao ya kijamii kwa kutaka achaguliwe mwanamke wa wa kumuoa tena.
Nuh aliweka wazi hisia zake hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika "nimejifunza mengi sana kwenye 'life style' yangu ya kimapenzi na najitoaga sana, ila siku ya mwisho naumizwa 'je unahisi mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu naye? leo nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili". Jambo hilo baadhi ya mashabiki zake walilichukulia tofauti na kupelekea kutoa maneno yenye ukakasi kwa kile wanachokidai kutoridhishwa na mwenendo wa msanii huyo kutotaka kutuliza akili yake baada ya kupata maumivu ya kimapenzi mfululizo kutoka kwa watu ambao alikuwa akijihusisha nao kimapenzi.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka