Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefunguka kwa kujitapa kuwa kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi 'Ngao ya Hisani' kesho atahakikisha anaifunga Yanga japo amepatwa na kitete cha kusema ni magoli mangapi ataifunga.
Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika 'gongo wazi' Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu.
"Game ya Yanga siku zote haiwagi rahisi kwa upande wowote kwa kuwa ni timu yenye wachezaji wazoefu wengi japo na sisi tunawachezaji wazoefu wengi kama wao, tunategemea mchezo wa kesho utakuwa mzuri pia tunamatumaini tutashinda", alisema Okwi.
Pamoja na hayo, Okwi aliendelea kwa kusema "nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na matokeo mazuri", alisisitiza Okwi.
Okwi ameanza tambwe hizo ikiwa imebakia siku moja kuchezwa kwa mechi ya watani wa jadi siku ya kesho (Jumatano) ambapo mchezo huo umekuwa ukisubiliwa na watu mbalimbali waweze kujua ni nani siku hiyo ataweza kumfunika mwenzak
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka