ROMA KUSHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA KESHO | BONGOJAMII

ROMA KUSHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA KESHO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Ikiwa imebakia siku kuelekea mtanange kwa mechi ya Ngao ya Jamii, rapa Roma Mkatoliki ambaye ni mshabiki namba moja wa klabu ya Simba amefunguka akidai siku hiyo atakuwepo uwanja wa Taifa kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji na mashabiki wa Simba.

Roma amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema siku hiyo timu ya Yanga ijiandae kwa kupokea kichapo kitakatifu.

"Wanangu wote mashabiki wa timu ya Simba tukutane Taifa kwa ajili ya kumng'oa huyu jamaa wa rangi ya njano (Yanga), tutamkalisha Stamina na wanae wote wanaoshabikia timu hiyo. Najua mashabiki wa Yanga hawataamini kitakachotokea sisi hatuongei sana",alisema Roma.

Katika hatua nyingine, msanii Stamina ambaye ni shabiki wa Yanga amedai timu hiyo haina upinzani na klabu yoyote kwa kuwa timu ya Yanga ndiyo imeshikilia rekodi ya ushindi mpaka sasa.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts