Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara ya juu Tazara Flyover katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba mwakani ili kuanza kutumika na wananchi ikiwa ni azma ya Serikali ya kupunguza foleni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati Rais wa Shirika la kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA), Dkt. Shinichi Kitaoka alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ya juu ambao unatekelezwa baina ya Tanzania na Serikali ya Japan.
Amesema ujenzi unaendelea vizuri na sasa umefikia asilimia 53, ambapo kasi ya ujenzi hui inaendelea ili barabara hii ikamilike kwa wakati na kuanza kutumika.
Aidha, Waziri Mbarawa ameishukuru Serikali ya Japan kwa kufadhili mradi huo ambao utasaidia kupunguza msongamano wa magari katika makutano hayo na hivyo kurahisisha usafiri kwa wakazi wanayoitumia barabara hiyo.
Kwa upande wake Rais, wa Rais wa JICA Dkt. Shinichi Kitaoka amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutaboresha mfumo wa miundombinu ya usafiri na JICA itahakikisha kazi ya Ujenzi huu inafanyika na kukamilika kwa wakati.
Mradi wa Tazara Flyover umefadhiliwa na Serikali ya Japani kupitia JICA na hadi kukamilika kwake utaghalimu shilingi Bilioni 99.
Imetolewa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka