BABA MZAZI WA LE MUTUZ AFUNGUKA HAYA JUU YA JESHI LETU LA POLISI | BONGOJAMII

BABA MZAZI WA LE MUTUZ AFUNGUKA HAYA JUU YA JESHI LETU LA POLISI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Baba Le Mutuz (Malecela) Afunguka mazito



Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini, wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya ikiwa ni pamoja na kuwatumika Watanzania wote kwa upendo moyo mmoja.


Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.
Mzee Malecela alisema; 


“Tulipopata uhuru na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alisema, Watanzania tumepata uhuru, hatuna uwezo wa kunyesha hela kama mvua kutoka mbinguni, umaskini utaendelea kuwepo.


“Lakini jambo moja la uhakika tunaloweza kumfanyia Mtanzania huyu, ni kuhakikisha tunapata heshima yake.


“Heshima ni kitu ambacho serikali inaweza kumpa kila Mtanzania…”

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts