CANADA YAFANYA MAAMUZI MAZITO, KUHALALISHA BANGI MWAKA UJAO | BONGOJAMII

CANADA YAFANYA MAAMUZI MAZITO, KUHALALISHA BANGI MWAKA UJAO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Matumizi ya bengi kwa kujiburudisha yatahalalishwa nchini Canada ifikapo tarehe mosi Julai mwaka 2018.


Serikali ya Canada itawasilisha mswada wa kuhalalisha bangi ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CBC.


Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha Liberal hivi majuzi walijulishwa kuhusu mswada huo.


CBC imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na serikali.


Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi wa kujiburudisha kwa watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18,.


opo kazi hilo pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea minne ya bangi na wamiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa.


Kwa mujibu wa CBS, serikali itasimamia kusambazwa wa bangi na kuwapa leseni wazalishaji.
Wabunge waidhinisha kilimo cha bangi


Ahadi wa waziri mkuu Justin Trudeau, ya kuhalalisha bangi imechochea uvumi katika sekta hiyo.


Wazalishaji kama makampuni ya Aphria, OrganiGram Holdings, na Canopy Growth, ambao ni wazalishaji wakubwa zaidi wa bangi ya kutibu, yamekuwa vipnzi kwa wawekezaji wa hisa.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts