BREAKING NEWS: IGP MPYA SIMON SIRRO KATANGAZA DAU NONO LA MILIONI 10 , KUHUSU MAUAJI YA KIBITI | BONGOJAMII

BREAKING NEWS: IGP MPYA SIMON SIRRO KATANGAZA DAU NONO LA MILIONI 10 , KUHUSU MAUAJI YA KIBITI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro kwa mara ya kwanza amefanya mazungumzo maalum na wanahabari jijini Dar es Salaam na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. 


“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.

Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.

“Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema 

==>Msikilize hapo chini akiongea


Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts