WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WABUNGE JUU YA SAKATA LA MCHANGA WA MADINI | BONGOJAMII

WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WABUNGE JUU YA SAKATA LA MCHANGA WA MADINI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji wa madini nchini kuondoa hofu ya kukosa haki zao kwani kamati ya pili iliyoagizwa kufanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (makinikia) bado haijakamilisha kazi yake.


Waziri Mkuu alisema hayo jana wakati akijibu swali la mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka, lililohoji kuhusu taswira ya Tanzania kimataifa hasa katika uwekezaji wa madini.


Majaliwa aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa kamati ya pili iliyoundwa kuangalia athari za kisheria, kisiasa na kimataifa kuhusu sakata la mchanga wa madini bado haijatoa ripoti yake.


“Watanzania wengi walikuwa na hofu, hata wabunge wengi katika serikali hii ya awamu ya tano mmekuwa mkizungumzia sakata la mchanga wa madini, lakini niwatoe hofu, Rais John Magufuli alifanya hayo kwa nia njema ya kulinda rasilimali za Taifa,” amliema


Waziri Mkuu aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa serikali itazingatia ushauri kutoka sekta nyingine kabla ya kuchukua hatua katika sakata hilo la mchanga wa madini.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts