CHAMA CHA WAMILIKI WA MABASI WAPINGA MASHINE ZA KIELETRONIKI KWENYE MABASI | BONGOJAMII

CHAMA CHA WAMILIKI WA MABASI WAPINGA MASHINE ZA KIELETRONIKI KWENYE MABASI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkutano Mkuu wa Chama cha wamiliki wa mabasi - TABOA umeazimia kwa kauli moja kupinga mpango wa matumizi ya mashine za kieletroniki katika ukatishaji wa tiketi kwa abiria wanaotumia mabasi hayo hadi pale watakapomaliza tofauti zao na serikali.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa TABOA, Abdalah Mohamed tofauti hizo ni zile zinatokana na changamoto ya matumizi ya mashine za kieletroniki ambapo ni lazima eneo husika kuwa na huduma za Internet ilihali huduma hiyo haipatikani vizuri maeneo yote nchini hivyo ipo hatari ya watu kushindwa kupata tiketi iwapo maeneo waliyopo hayana huduma hiyo.

Kutokana na hali hiyo wajumbe wa mkutano huo mkuu wa TABOA wakaingia katika majadiliano makali huku baadhi wakitaka mkutano mkuu mwingine wa dharura uitwe huku mawaziri wenye dhamana ya ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano na yule mwenye dhamana ya fedha na mipango na wasaidizi wao wawepo ili kulijadili suala hilo na kulipatia ufumbuzi.

Hata hivyo mkutano huo ukaunga mkono hoja ya Naibu Katibu mkuu wa TABOA, Issa Nkya ya kutolewa wiki moja kwa kamati maalum ya TABOA ambayo ilikuwa imeundwa kufuatilia suala hilo wamalizane na mamlaka ya mapato Tanzania -TRA kupitia kamishina mkuu wa kodi na ikishindikanika wachukue hatua nyingine.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts