MAAGIZO YA WAZIRI UMMY KWA WANANCHI | BONGOJAMII

MAAGIZO YA WAZIRI UMMY KWA WANANCHI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Wananchi wameagizwa kufuata utaratibu wa sera unaotaka wananchi kupata matibabu katika hospitali za Rufaa ni lazima awe ameandikiwa rufaa na siyo kila mtu aende moja kwa moja kwenye hospitali hizo.

Hayo yamezungumzwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na watumishi wa sekta ya afya wa Mkoa na Wilaya mkoani Rukwa ambapo ameagiza Manispaa ya Sumbawanga kuongeza kujenga vituo vya afya ili hospitali ya Rufaa ya mkoa ibaki kutoa huduma za kibingwa .

"Serikali inaboresha hospitali za Rufaa za Mkoa kwa ajili ya huduma za kibingwa hivyo hospitali hizo ziweze kutoa huduma za kimatibabu ya kibingwa kwa watu wenye uhitaji huo," alisema

Pamoja na hayo Waziri Ummy amesema kulingana na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini ni vyema na mkoa kujenga vituo vitakavyoweza kutoa huduma kwa wananchi waliopo maeneo husika kuliko kujenga hospitali ya Wilaya ambayo wananchi waliopo maeneo ya mbali wapate huduma za afya huko huko karibu na huduma hizo ziwe bora.

“Fanyeni maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wa wilaya yenu ili muwasogezee huduma watu wenu, kwa Wilaya ya Nkasi mnatakiwa kujenga hospitali ya wilaya ya serikali ambapo Wizara itawasaidia kutoa milioni 350 kati ya 650 ambazo zitajenga wodi ya wazazi, maabara pamoja na nyumba moja ya mtumishi" aliongeza.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts